LULU AFUNIKA CHUO


Kichwa! Staa bei mbaya wa sinema za Kibongo aliyejizatiti katika masomo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ anadaiwa kuwafunika kimasomo wanafunzi wenzake katika Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) kilichopo Magogoni-Posta jijini Dar.



Staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ akipozi.

Akizungumza hivi karibuni chuoni hapo, mmoja wa wanafunzi wanaosoma na mwigizaji huyo aliyeomba hifadhi ya jina lake alisema Lulu amekuwa akihudhuria vizuri darasani na kufanya vyema kwenye masomo yake mbalimbali zaidi ya wanafunzi wengi anaosoma nao.
“Lulu yupo vizuri sana kimasomo, anawapita hadi wanafunzi wengine. Mahudhurio yake ni mazuri na anafanya mitihani yake na kufaulu.

“Anavaa nguo zinazostahili na hapa chuoni kila mwanafunzi anampenda kwa sababu yupo ‘peace’ ile mbaya,” alisema mnyetishaji huyo na kusisitiza kuwa msanii huyo haishi kama supastaa.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright VIJIMAMBOZI Published.. Blogger Templates
Back To Top