Lulu Atoboa Sababu ya Kutofanya ‘Movie’kwa Mwaka Mzima


Staa wa Bongo Movies, Elizabeth Michael,’Lulu’amefunguka sababu ya kutofanya filamu kwa mwaka mzima kuwa alikuwa bize na shughuli zingine ikiwemo masomo.

Akizungumza na Clouds Fm,alisema kuwa mwaka jana wote alikuwa ‘host’ kwenye mashindano ya kutafuta vipaji vya uigizaji (Tanzania Movie Talents) ambayo ilifanyika karibu mikoa yote,pia alikuwa bize na masomo katika chuo cha Magogoni akichukua kozi ya Public Administration.

‘’Mwaka jana wote sikufanya filamu kabisa kutokana na kuwa bize kwenye shindano la kutafuta vipaji vya uigizaji na pia shule nayo ilinibana kwahiyo sikuwa na muda wa kufanya filamu,’alisema Lulu.

Aidha alisema kuwa kwa sasa ameingia mzigoni kufanya filamu yake mpya ambayo hajaipa jina bado chini ya kampuni yake ya Proin Promotion ambayo itakuwa na wasanii mbalimbali kama Dude na wengineo.

‘Filamu hii inahusu maisha,mapenzi na komedi kidogo na kwa sasa hivi nitakuwa natoa filamu mbili kwa mwaka ndiyo utaratibu niliojiwekea,’aliongeza Lulu.

Cloudsfm.com

VODACOM TANZANIA YAZINDUA PROGRAMU YA MZIIKI NDANI YA ZARI WHITE PARTY

 

Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa (katikati) akimsikiliza jambo Msanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya Diamond Platinumz (kulia) na balozi wa Mziiki ambayo ni programu ya simu za mkononi (mobile app) ya Vodacom Tanzania iliyozinduliwa jana wakati wa Zari White Party iliyofanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam jana.

Msanii wa muziki wa Bongo Flavor Diamond Platinumz (wa pili kutoka kushoto) na balozi wa Mziiki ambayo ni program ya simu za mkononi (mobile app) ya Vodacom Tanzania akiwaonyesha…



Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa (katikati) akimsikiliza jambo Msanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya Diamond Platinumz (kulia) na balozi wa Mziiki ambayo ni programu ya simu za mkononi (mobile app) ya Vodacom Tanzania iliyozinduliwa jana wakati wa Zari White Party iliyofanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam jana.

Msanii wa muziki wa Bongo Flavor Diamond Platinumz (wa pili kutoka kushoto) na balozi wa Mziiki ambayo ni program ya simu za mkononi (mobile app) ya Vodacom Tanzania akiwaonyesha program hiyo waandishi wa habari (hawamo pichani). App hiyo inawaletea wateja burudani ya muziki kiganjani. Wengine katika picha ni Maofisa Mawasiliano wa kampuni hiyo, Abigail Ambweni(wa kwanza kushoto) na Glory Mtui.

Ofisa Mawasiliano na Matukio wa Vodacom Tanzania, Abigail Ambweni (kulia) akihojiwa na mtangazaji wa Clouds TV wakati wa uzinduzi wa program ya Mziiki ambayo ni program ya simu za mkononi (mobile app) ya Vodacom Tanzani.

MARIAH CAREY: SASA NAWEZA KUPENDA

 

 
Staa wa muziki wa Pop, Mariah Carey

STAA wa muziki wa Pop, Mariah Carey ameweka bayana kuwa sasa anaweza kupenda tena baada ya kuachana na mzazi mwenzake, Nick Cannon.

Mariah Carey akiwa na aliyekuwa mumewe Nick Cannon.

Staa huyo alisema kuwa lolote linawezekana chini ya jua na kwamba akipata anayempenda, hatajizuia kuwa naye hadharani.Akizungumza na tovuti ya people.com, staa huyo alisema kwamba hatasita kujiachia…





Staa wa muziki wa Pop, Mariah Carey

STAA wa muziki wa Pop, Mariah Carey ameweka bayana kuwa sasa anaweza kupenda tena baada ya kuachana na mzazi mwenzake, Nick Cannon.

Mariah Carey akiwa na aliyekuwa mumewe Nick Cannon.

Staa huyo alisema kuwa lolote linawezekana chini ya jua na kwamba akipata anayempenda, hatajizuia kuwa naye hadharani.Akizungumza na tovuti ya people.com, staa huyo alisema kwamba hatasita kujiachia na mtu atakayempenda kwani sasa hana kizuizi.

“Nikiwa kama binadamu nina haki ya kupenda na nikimpata ninayempenda, kila mtu atamjua kwa kuwa sitamficha. Hata akitaka kunioa pia nipo tayari,” alisema Mariah Carey mama wa watoto wawili, Oacha Monroe na Morocana aliowapata alipokuwa na mumewe Cannon.Staa wa muziki wa Pop, Mariah Carey



STAA wa muziki wa Pop, Mariah Carey ameweka bayana kuwa sasa anaweza kupenda tena baada ya kuachana na mzazi mwenzake, Nick Cannon.

Mariah Carey akiwa na aliyekuwa mumewe Nick Cannon.

Staa huyo alisema kuwa lolote linawezekana chini ya jua na kwamba akipata anayempenda, hatajizuia kuwa naye hadharani.Akizungumza na tovuti ya people.com, staa huyo alisema kwamba hatasita kujiachia na mtu atakayempenda kwani sasa hana kizuizi.

“Nikiwa kama binadamu nina haki ya kupenda na nikimpata ninayempenda, kila mtu atamjua kwa kuwa sitamficha. Hata akitaka kunioa pia nipo tayari,” alisema Mariah Carey mama wa watoto wawili, Oacha Monroe na Morocana aliowapata alipokuwa na mumewe Cannon.

HIZI NDIO BEI ZA KINGWENDU KWENYE VIDEO ZA WASANII

 
Staa mkongwe kwenye uchekeshaji, Kingwendu amesema kuonekana kwenye video za muziki za wasanii ni moja ya biashara zake anazozipa uzito.

Kingwendu ameonekana kwenye video kadhaa ikiwemo ile ya wimbo wa Yamoto Band.
Akiongea na 255 ya XXL kupitia kituo cha redio cha Clouds FM, Kingwendu alisema kabla hajakubali kufanya video, huangalia kwanza wimbo huo una ujumbe gani.
“Inategemea kwanza na video gani, kama ni movie au muziki kama muziki, naangalia kwanza ameimba nini na huo wimbo una ujumbe gani. Mfano ujumbe kama wa wimbo ule wa Yamoto Band,” alisema.

“Video ya muziki nafanya kuanzia laki tano hadi milioni moja hiyo ni kwa underground, hapo atakuwa amelialia ndio nawafanyia bei hiyo. Ila supastar mwenzangu namfanyia bei rahisi maana najua ipo siku na miye nitamwitaji. Cha muhimu tufanye tu kazi kwa ushirikiano.”
Bongo5

'TUSIMUONEE HURUMA KABISA SHILOLE KUMCHAPA VIBAO NUHU MZIWANDA "...soma hapa..




Mziwanda wala tusimuonee huruma. Inaonesha kweli anapenda kupigwa kama Snura anavyosema! mnafanya kazi bure kuwashauri. Hapo kitakochotokea Mziwanda anajiharibia kazi yake, lets be honest hivi anavyopigwa pigwa hovyo kuna mwanaume atasikiliza au kuangalia nyimbo zake? Noo make watasema "yule fala tu mwanaume gani anapigwa na mpenzi wake?" Halafu kwa wasichana watasikiliza nyimbo zake vile tu kana sura nzuri si unajua sie wadada tunavutiwa na vitu vidogo tu!! Halafu Mziwanda nahisi anadhani akimuacha Shilole ndo amekwisha kimuziki itabidi ang'ang'anie hapo hapo.... Mpaka atakapochukua maamuzi kama mwanaume akajitambua ndo watu wote wataikubali kazi yake..lkn sasa hapana! ..

Ni Maneno ya Mwanamuziki Snura wa Majanga....Je Unakubaliana nae ?

MAJANGA: WATU WAMVAA AUNT

 
KUFUATIA madai kuwa staa wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel amejifungua, ndugu, jamaa na marafiki kibao walijazana nyumbani kwake, Mwananyamala jijini Dar es Salaam juzi Alhamisi ili kumpa pongezi, lakini walipokuta habari tofauti walimvaa na kumlaumu kwa kuwadanganya.

Staa wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel.

Jumatano usiku katika mtandao wa kijamii wa Instagram, msanii Aunt Ezekiel ambaye ni mke wa mtu aliyepata ujauzito mumewe akiwa jela, alitupia picha ikimuonyesha akiwa na kitoto kichanga, ambacho watu wengi waliamini ni wa kwake, hasa kwa vile katika siku za hivi karibuni ameonekana kupunguza mitoko.

Watu wa karibu wa muigizaji huyo ambaye hivi sasa ana uhusiano wa kimapenzi na mcheza shoo wa Diamond Platnumz aitwaye Iyobo, walikwenda nyumbani kwake kwa ajili ya kumpongeza, lakini walipatwa na mshangao baada ya kumkuta akiwa na tumbo lake kama kawaida.

“Sisi tulijua mwenzetu amejaaliwa kujifungua salama, sasa jambo la kushangaza wenzake tumekuja kwa furaha tunakutana na mtu mzima kabisa, hivi aliwaza nini kuweka picha ile katika mtandao na wala asiseme ukweli wa kinachoendelea,” shoga mmoja wa muigizaji huyo aliliambia gazeti hili nje ya nyumba yake, lakini akaomba jina lake lihifadhiwe gazetini.

Mmoja wa marafiki waliodaiwa kufika wakiwa wamekasirika nyumbani kwa Aunt, alikuwa ni shosti yake Wema Sepetu, aliyeshangaa sababu za kutoambiwa mapema kuhusu ukweli wa ishu hiyo.

“Nilishtuka kweli, nikasema inakuwaje Aunt apate mtoto halafu mimi nione kwenye mitandao ya kijamii? Nafika hapa kumbe hamna lolote Aunt naye hakufanya fair bwana,” alisema Aunt.Ujauzito wa Aunt kwa sasa unadaiwa kukaribia mwezi wa saba, hivyo wengi waliposikia amejifungua walidhani amepata kiumbe njiti.

"MUME WA ZARI ANATAKA KUNIOA "...WEMA


 MAMBO hadharani! Supastaa wa Bongo, Wema Sepetu ‘madam’ ameanika siri zilizojificha nyuma ya pazia kati yake na aliyekuwa mume wa mwanamuziki nyota wa Uganda, Zarina Hassan ‘Zari’, Ivan Semwanga, kuwa anataka kumuoa, Risasi Jumamosi lina full stori.

Supastaa wa Bongo Movie, Wema Sepetu ‘madam’.

WALIANZIA KUKUTANA SAUZ
Katika mazungumzo yake exclusive na mwanahabari wetu juzi jijini Dar, Wema alianza kwa kuweka bayana kwamba, mawasiliano yake na Ivan yalianzia nchini Afrika Kusini wakati alipokwenda kikazi, Februari, mwaka huu.

“Nilikwenda na Ommy Dimpoz (Faraj Nyembo). Tulikuwa na project yake lakini tulipokuwa kule, Ivan na marafiki zake walisikia kuwa mimi nipo, wakatuomba sana kupitia kwa wenyeji wetu kuwa wanataka kutuona na kutoka nao out pamoja.”

ALIBANA, AKALEGEZA
“Mimi nilikuwa bize sana na kazi zangu, awali niliwaambia kuwa hatutaweza lakini baadaye walitubahatisha klabu, wakaomba kukaa na sisi, mwishoni ilibidi tuwakubalie lakini kwa masharti ya kuwa wasije wakatuzushia lolote.

“Tulikubali, wakaja, tukakaa nao meza moja, tukabadilishana mawasiliano kama marafiki. Lakini baadaye tukaona wanaongezeka, sikupenda vurugu ya watu wengi, mimi na Ommy tukaamua kuondoka zetu,” alisema Wema.

IVAN AANZA ‘KUIMBISHA’
Akizidi kumwaga siri zake na mwanaume huyo, Wema alisema baada ya yeye kumaliza project yake nchini humo, alirejea Bongo na ndipo Ivan alipozidisha ufundi wa kumuomba urafiki wa kimapenzi huku akimuahidi mambo mengi ya muhimu.

Msikie Wema: “Baada ya hapo tulikuwa tunawasiliana na Ivan, lakini kadiri siku zilivyokuwa zikisonga mbele, nikaona mwenzangu anaanza kunitongoza, tena akawa anaendelea kila siku licha ya mimi kutomkubalia.”

Aliyekuwa mume wa mwanamuziki nyota wa Uganda, Zarina Hassan ‘Zari’, Ivan Semwanga.

AHADI NI MAGARI, NYUMBA
Wema alizidi kutiririka kuwa, hadi sasa (mapema wiki hii), Ivan hajakata tamaa, amekuwa akiendelea kumtongoza na kumuahidi ahadi mbalimbali.
Endapo atamkubalia na kuwa baby wake, basi atampa nyumba ya kifahari na magari ya kisasa (awe kama Zari).

Wema anakiri mwenyewe: “Alianza kuniahidi maisha mazuri, nyumba, magari na hata kunioa lakini kimsingi sijamkubalia kwani sijamwamini kama ana mapenzi ya dhati. Nahisi kuna kitu nyuma yake kinamsukuma kufanya hivyo.”

ATAKIWA KUTOICHEZEA BAHATI
Kwa mujibu wa chanzo makini, kuna uwezekano mkubwa Wema akaingia kwenye himaya ya Ivan kutokana na ushawishi wake mkubwa anaoufanya kwa madam huyo, hivyo akawa tajiri mkubwa.
“Wema kwa sasa hatakiwi kuichezea bahati kwani Ivan ni mtu anayejiheshimu. Ana biashara zake kubwakubwa, hivyo suala la fedha za maisha hazimpigi chenga,” kilisema chanzo hicho.

WEMA KUWA KAMA MCHARO?
Akizungumzia suala hilo, rafiki wa karibu wa Wema ambaye hakupenda jina lake liandikwe gazetini, alisema licha ya Wema kutokubali ombi la Ivan lakini anaamini siku si nyingi atakubali na atakuwa vizuri kiuchumi kuliko alivyo sasa.

“Jamaa yupo serious na ndoa, Wema atakubali tu na ndoa itafungwa. Mtoto wa kike sasa atakuwa si wa magari ya kawaida, full kubadilisha, atakuwa mtamu kama mcharo,” alisema rafiki huyo.

KINACHOMPA WASIWASI WEMA
Rafiki huyo aliendelea kusema kuwa, Wema ana wasiwasi kwamba, mapenzi ya Ivan kwake ni kwa ajili ya kulipa kisasi kwa sababu ya Diamond (aliyekuwa mpenzi wa Wema) sasa yuko na Zari (aliyekuwa mke wa Ivan).

“Kwa hiyo Wema ana wasiwasi kwamba, siku akimkubalia tu Ivan akapiga naye ngwara, biashara itakuwa imeishia hapo kwani nia ya kisasi ya mwanaume huyo itakuwa imekamilika,” alisema rafiki huyo.

FAIZA: HAKUNA STAA MWENYE FIGA KAMA YANGU

 
MZAZI mwenziye na Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’, Faiza Ally amesema kuwa hakuna staa yeyote hapa Bongo mwenye figa kama yake ya kuweza kuvaa ‘bikini’ na kujiachia kama yeye.

Mzazi mwenziye na Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’, Faiza Ally.

Akifunguka na Centre Spread, Faiza alisema kuwa wapo mastaa wengi wembamba lakini maumbo yao hayana mvuto hasa wakivaa bikini huku akitolea mfano wa Nancy Sumari na Jacqueline Patrick.



“Ukitaka kujua kama una umbo zuri tena la kimataifa wewe jaribu kuvaa bikini uone, ndiyo utajijua ni mrembo kiasi gani. Najitambua navutia kiasi gani nikivaa bikini,” alisema Faiza.

JUX BADO UNABISHA UHUSIANO WAKO NA VANESSA

BAADA ya kukataa mara kwa mara juu ya uhusiano wao wa kimapenzi, hatimaye wasanii Juma Mussa ‘Jux’ na Vanessa Mdee ‘Vee Money’ juzikati walikutwa katika mkao wa kimahaba kiasi cha kuwafanya mashabiki kujiuliza kama mkali huyo wa kibao cha Uzuri wako anaweza kuendelea kubisha.

Wabongo Fleva Juma Mussa ‘Jux’ na Vanessa Mdee ‘Vee Money’ wakila ujana.

Wawili hao walikutwa wamepakatana wakati wa onyesho la kutambulisha video za wakali wa Bongo Fleva, lililofanyika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya Escape One, Mikocheni jijini Dar.

Vee Money alithibitisha kuwa wao ni wapenzi mbele ya umati alipokuwa stejini akiimba naye pamoja na Barnaba wimbo walioshirikiana unaojulikana kwa jina la Siri, akisema anampenda sana Jux na kuwafanya mashabiki kumshangilia kwa nguvu.

Juma Mussa ‘Jux’ akipozi.

Baada ya Vanessa kumaliza shoo yake, ukafuata wakati wa Jux ambaye alipomaliza na kurudi nyuma ya jukwaa, Vee alimpisha mvulana huyo akae kitini kisha yeye akamkalia, jambo lililotosha kuwaaminisha watu mapenzi yao.

“Njooni muone jamani Vanessa kapakatwa na Jux tena hawana hata wasiwasi wenyewe wamejiachia kama hawapo vile, watakuwa ni wapenzi tu kwa maana huwa wanaficha sana,” alisikika akisema shabiki.
Hawakuishia hapo, kwani waliendelea kuoneshana mahaba mpaka walipoondoka katika viwanja hivyo.

WEMA AMTUSI SHEMEJI WA ZARI

 
 
KIMENUKA! Beautiful Onyinye, Wema Sepetu ‘Madam’ amemporomoshea matusi mazito shemeji wa Zarina Hassan ‘Zari’, King Lauwrance akidai amemuudhi sana kwa kitendo cha kuvujisha picha inayomuonesha akiponda raha nchini Afrika Kusini ‘Sauz’ na mume wa Zari, Ivan Semwanga, Risasi Mchanganyiko linakupa mchapo kamili.


Beautiful Onyinye, Wema Sepetu ‘Madam’.

Mwishoni mwa wiki iliyopita, Wema na staa wa Bongo Fleva, Omari Nyembo ‘Ommy Dimpoz’ walikwenda Sauz kurekodi video ya wimbo wa msanii huyo ambao jina lake bado halijafahamika mara moja ndipo baadae picha ya Ivan, Wema na King Lawrence ilipovuja na kuzua gumzo.

TUJIUNGE NA CHANZO
Kwa mujibu wa chanzo chetu kilichokuwa Sauz, baada ya Wema na Ommy kutua nchini humo na ‘project’ hiyo ya video, King Lawrance alidaiwa kuandaa mpango kabambe wa kuhakikisha kwa namna yoyote wanaonana na Wema kisha kupiga naye picha ambayo akiivujisha mtandaoni kila mtu ataamini wamefanya malipizi kwa zilipendwa wa Wema, Nasibu Abdul ‘Diamond’ ambaye amemnyakua Zari, mke wa Ivan.

“Ilikuwa ni mpango wa malipizi, King na Ivan walikuwa wanaumia moyoni kumuona Diamond anatoka na Zari wakati wao wana fedha kuliko Diamond hivyo waliposikia mtoto wa kike (Wema) yupo Sauz wakasema watadili naye hadi kieleweke, iwe ni kwa kufanikisha zoezi la kutoka naye kimapenzi au hata kupiga picha ambazo zikisambaa mitandaoni, watu watajua kwamba wamefanya malipizi,” kilisema chanzo chetu.

King Lauwrance (kushoto) akipozi na Ivan( aliyekuwa mume wa Zari).


KING AFANIKIWA KUIVUJISHA
Chanzo hicho kilizidi kumwaga ubuyu kuwa, baada ya kufanya project, Ommy na Wema usiku walikwenda katika moja ya klabu kula bata ndipo King na Ivan walipozama na kufanikiwa kupata picha na Wema wakiwa katika kochi moja kisha akaitupia katika mtandao wa Istagram.

“Wema aliwachukulia kama washkaji, hakujua jamaa walikuwa na lao kichwani, walipofanikiwa kupata picha tu, wakaitupia mtandaoni fasta na kufanya Wema atukanwe na watu,” kilisema chanzo hicho.

WEMA ACHARUKA
Baada ya picha za Wema na Ivan kusambaa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii, mwandishi wetu alimtafuta Wema kwa njia ya simu ambapo alimcharukia King kwa matusi mazito ambayo kimaadili hayandikiki gazetini hata mtandaoni.

Zarina Hassan ‘Zari’ akipozi.


“Yule ni...(tusi) ameniboa kweli...(tusi) unajua vitu vingine vya kipuuzi kabisa, wanatafuta kiki zisizokuwa za msingi wa...(tusi)” alisema Wema.Wema alisisitiza kuwa hataki kumzungumzia sana King kwani anaamini akifanya hivyo atamuongezea umaarufu ambao amekuwa akiutafuta muda mrefu.

King Lawrence amekuwa akimtusi Diamond mara kwa mara kwenye mitandao ya kijamii huku akionesha jeuri ya fedha kwa kile kinachoonekana kuumia kwake roho kwa kijana wa Tandale kumchukua shemeji yake Zari, aliyezaa na Ivan watoto watatu.

MAKUBWA HAYA!:HIRIZI YAKUTWA KWA WEMA


IMANI za kishirikina? Mshangao wa aina yake umetokea nyumbani kwa Miss Tanzania 2006 asiyechuja, Wema Abraham Sepetu ‘Madam’ baada ya kutupiwa hirizi getini kwake, Risasi Mchanganyiko lina stori kamili.

Wananchi wakishuhudia hirizi getini kwa Miss Tanzania 2006 asiyechuja, Wema Abraham Sepetu ‘Madam’.

Tukio hilo lililokusanya watu wapenda ‘ubuyu’ lilijiri alfajiri ya Jumamosi iliyopita, nyumbani kwa mlimbwende huyo, Kijitonyama-Bwawani jijini Dar baada ya mapaparazi wetu kutonywa juu ya uwepo wa tukio hilo.

TUJIUNGE NA CHANZO
“Njooni hapa kwa Wema tumekuta mfuko mweusi wa nailoni, ndani yake una hirizi, nazi zimeandikwa maandishi ya Kiarabu huku zikiwa zimevunjwavunjwa na pia kuna picha ya Diamond ndani yake,” kilisema chanzo hicho.

MAPAPARAZI WATIA TIMU
Mapaparazi wetu ambao walikuwa kwenye mizunguko yao kikazi, walitumia usafiri wa pikipiki kwenda nyumbani hapo ambapo ndani ya dakika ‘sifuri’ walikuwa wameshafika na kukuta vitu hivyo vikiwa vimezunguka na mashuhuda.

Wananchi wakizitazama kwa karibu zaidi hirizi hizo.

KILA MTU ASEMA LAKE
Wakati mapaparazi wetu walipokuwa wakidadisi juu nani aliyetupa kifurushi hicho na sababu za kufanya hivyo, mashuhuda hao kila mmoja alieleza lake.
“Sisi hatujui aliyetupa inaonekana atakuwa alikuja usiku sana lakini inaonesha mtupaji atakuwa anataka Wema na Diamond warudiane na ndiyo maana ameambatanisha na picha ya Diamond,” alisikika shuhuda mmoja huku mwingine akidakia:
“Aliyetupa hapa atakuwa ameweka zindiko ili Diamond asirudiane tena na Wema. Atakuwa anataka Diamond aendelee na Zari.”

Katika hali ya kushangaza, mlinzi wa kampuni moja inayolinda nyumbani kwa mlimbwende huyo, aliupiga teke na kuusambaratisha mfuko uliokuwa umehifadhi vitu hivyo pamoja na hirizi.

MAPAPARAZI WAMGONGEA WEMA
Ili kutaka kujua Wema amelichukuliaje tukio hilo, mapaparazi wetu waligonga geti la Wema ambapo alitoka binti mmoja ambaye hakutaka kujitambulisha jina lake na kuzungumza pasipo kufungua geti akiwa anachungulia kupitia uwazi mdogo uliopo getini hapo.

Hizi ndizo hirizi zilizokutwa getini kwa Wema zikiwa na picha ya 'Diamond'.


“He mimi sifungui, Madam (Wema) hayupo kwanza naogopa hivyo vitu si vya kawaida, mimi nakwenda zangu ndani,” alisema binti huyo na kutoweka.

APIGIWA SIMU
Mapaparazi wetu walimvutia waya Madam ambapo kilongalonga chake kiliita bila ya kupokelewa, kesho yake (Jumamosi) mapaparazi walitia timu tena nyumbani hapo na kuambiwa Madam hayupo huku simu yake ikiwa haipatikani.

WAHARIRI MZIGONI
Juzi, Jumatatu wakati gazeti hili lilipokuwa linakwenda mitamboni, wahariri wa gazeti hili walifunga safari hadi nyumbani kwa Wema na kugonga getini kwake ambapo alitoka mtu wa karibu na Wema, Petit Man. Mazungumzo yakawa hivi:
Petit: Yeah karibuni.

Staa wa filamu Bongo, Wema Sepetu.


Wahariri: Tumekuja kumuona Madam, tumemkuta?
Petit: Mna miadi naye?
Wahariri: Hatuna ila we mwambie wahariri wa Global Publishers wanakuita.
Petit: Ok subirini.
(Baada ya sekunde 30)

WEMA, PETIT WATOKA NA GARI
Wakati wahariri wakiendelea kusubiri, Wema na Petit walitoka getini wakiwa na gari aina ya Murano (lile la alilopewa Diamond) ndipo wakashusha kioo ili waweze kuzungumza nao.
Mhariri: Mambo? Vipi mzima?
Wema: Mzima niambie.

Mhariri: Dakika mbili kidogo basi tuongee.
Wema: Nina haraka lakini.
Mhariri: Hata dakika moja. Ni hivi, kuna picha tumeletewa na mapaparazi wetu zinaonesha juzi hapa nyumbani kwako kuna mfuko ulitupwa hapa ukiwa na hirizi na mazagazaga yanayosadikiwa kuwa ni ya kishirikina.

Mkali wa Bongo Fleva, 'Diamond Platnumz'.


Wema: (Kwa mshtuko) Haaaah! Hapa...kwa...ngu.
Mhariri: Hapa kwako ndiyo tena ndani yake kuna picha ya Diamond.
Wema: Kwa kweli mimi...sijui...hata sielewi kama kuna kitu kama hicho kimetokea nyumbani kwangu.

MABAKI YAONEKANA
Wakati wahariri wakiendelea na mazungumzo na Wema, waliona mabaki ya vipande vya nazi pembeni ya geti hilo na kumuonesha Wema ambaye alizidi kutaharuki.
“Haaah! Kweli jamani vipande vya nazi...sawa lakini mimi imani yangu haiamini hivi vitu,” alisema Wema.
Baada ya mazungumzo hayo, wahariri walimuaga Wema huku akiwa katika hali ya sintofahamu!

LULU AFUNIKA CHUO


Kichwa! Staa bei mbaya wa sinema za Kibongo aliyejizatiti katika masomo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ anadaiwa kuwafunika kimasomo wanafunzi wenzake katika Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) kilichopo Magogoni-Posta jijini Dar.



Staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ akipozi.

Akizungumza hivi karibuni chuoni hapo, mmoja wa wanafunzi wanaosoma na mwigizaji huyo aliyeomba hifadhi ya jina lake alisema Lulu amekuwa akihudhuria vizuri darasani na kufanya vyema kwenye masomo yake mbalimbali zaidi ya wanafunzi wengi anaosoma nao.
“Lulu yupo vizuri sana kimasomo, anawapita hadi wanafunzi wengine. Mahudhurio yake ni mazuri na anafanya mitihani yake na kufaulu.

“Anavaa nguo zinazostahili na hapa chuoni kila mwanafunzi anampenda kwa sababu yupo ‘peace’ ile mbaya,” alisema mnyetishaji huyo na kusisitiza kuwa msanii huyo haishi kama supastaa.

PARTY YA AMANDA, FULL KUDENDEKA


Staa wa filamu za Kibongo, Tamrina Poshi ‘Amanda’ akimlisha keki rafiki yake, 'wastara'.


Na Hamida Hassan/Ijumaa
Staa wa filamu za Kibongo, Tamrina Poshi ‘Amanda’ hivi karibuni alifanyiwa pati ya bethidei ambapo kwenye zoezi la kuwalisha keki mashosti zake, aliwashangaza watu kwa kusema wote atawalisha kwa mdomo ‘staili ya kudendeka’.

‘Amanda’akiwalisha keki mashosti zake.

Pati hiyo ilifanyika juzikati kwenye Ukumbi wa Tamigamiga, Mbezi Beach jijini Dar ambapo mbali na staili hiyo ya kulishana keki, eneo la tukio lilitawaliwa na vituko kutokana na mastaa wengi kuwa bwii.

‘Amanda’akipozi na mdogo wake anayefahamika kwa jina la Sabrina.

Akizungumzia sherehe hiyo Amanda alisema: “Ilikuwa ni siku muhimu sana kwangu na nilifarijika kuona wasanii wengi kama vile Riyama, Esha Buheti, Wastara na wengineo wamejitokeza kufurahi na mimi. Ila kulishana keki vile ni staili ya kinjiwanjiwa, hahaaa!”

MAJANGA: DAVINA AKIRI KUWA WAIGIZAJI WENGI WA KIKE WANAJIUZA

Muigizaji mkongwe wa filamu na moja kati ya waasisi wa Kaone Sanaa Group, Halima Yahya ‘Davina’ amekiri kuwa ndani ya tasnia yao, kuna waigizaji wengi wa kike wanajiuza kwa maslahi yao binafsi.

Akipiga stori na paparazi wa GPL, Davina alisema wasanii wanaofanya hivyo ni wale wasio na nia ya dhati, wapo kwenye tasnia kwa ajili ya kuuza sura na kujinadi kwa mapedeshee.


“Tatizo ni kwamba wasanii tumekutana kila mmoja ana tabia zake na ni ngumu kujua undani wa mtu kwa kumtazama mara moja, sasa utakuta mtu yupo radhi aombe kucheza filamu hata bure kwa kuamini kwamba ataonwa na wanaume wenye pesa zao, na kweli inakuwa hivyo kwani wanapowatokea hawakatai, kimsingi wanatuchafua sana sisi ambao tupo serious na kazi,” alisema Davina.

ZARI UTUPIA NENO LA DIAMOND INSTAGRAM!

 
Mwanadada matata Zarina Hassan 'Zarithebosslady', ametupia neno la kumtakia kila kheri mpenzi wake Diamond Platnumz katika shoo yake ya leo usiku. Takriban dakika 45 zilizopita, Zari ametupia kwenye akaunti yake ya Intagram maneno yasemayo:Usiku huu nakutakia kila la kheri, nipo pamoja nawe kiroho...mahabbat hayo, lol!

YAMOTO BAND WAACHIA VIDEO YAO MPYA YA "NITAKUPWELEPWETA" ==>>KUWA WAKWANZA KUTAZAMA HAPA


Style ya muziki wanaoufanya imewafanya kupanda mashabiki wa umri tofauti,Yamoto Band wametuletea video yao mpya hii inaitwa Nitakupwelepweta,imeongozwa na Adam Juma.

Bonyeza play kutazama 

SOMA ALICHOKISEMA DIAMOND KUHUSU TIGO NA WASANII>>

 

PICHA ZILIZOANGALIWA NA WATU WENGI ZAIDI HUKO INSTAGRAM

 

Anajulikana kwa jina la CORAZON KWAMBOKA almaarufu kama MS.BIG BOOTY kutoka kenya akiwa na umri wa miaka 22 tu mpaka akiwa amejizolea umaarufu mkubwa kutoka na umbo lake lilivyo,

Nimekuletea picha zake hizi zikionyesha mapaja yake yalivyo














" INGAWA NIMEZAA MVUTO BADO NINAO"...FAIZA


Mwigizaji wa filamu alietoa kali ya mwaka jana kwa kuvaa Diaper wavaayo watoto kuhifadhi haja zao maarufu kama ‘pempasi’ kwenye kusherekea siku yake ya kuzaliwa, Faiza Ally leo ameibuka na picha akiwa ufukweni amevalia vinguo vya kuogelea huku pembeni akiwa na mtoto wake nakudai kuwa bado ana mvuto hata baada ya kuzaa mtoto.
“Hata baada ya kuzaa naona niko sexy ile mbaya kudadadeki!!!!” Faiza aliandika
Haya hebu jionee na umwambie kitu mama huyu mwenye mvuto.
Older Posts
© Copyright VIJIMAMBOZI Published.. Blogger Templates
Back To Top