BAADA ya kukataa mara kwa mara juu ya uhusiano wao wa kimapenzi, hatimaye wasanii Juma Mussa ‘Jux’ na Vanessa Mdee ‘Vee Money’ juzikati walikutwa katika mkao wa kimahaba kiasi cha kuwafanya mashabiki kujiuliza kama mkali huyo wa kibao cha Uzuri wako anaweza kuendelea kubisha.
Wabongo Fleva Juma Mussa ‘Jux’ na Vanessa Mdee ‘Vee Money’ wakila ujana.
Wawili hao walikutwa wamepakatana wakati wa onyesho la kutambulisha video za wakali wa Bongo Fleva, lililofanyika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya Escape One, Mikocheni jijini Dar.
Vee Money alithibitisha kuwa wao ni wapenzi mbele ya umati alipokuwa stejini akiimba naye pamoja na Barnaba wimbo walioshirikiana unaojulikana kwa jina la Siri, akisema anampenda sana Jux na kuwafanya mashabiki kumshangilia kwa nguvu.
Juma Mussa ‘Jux’ akipozi.
Baada ya Vanessa kumaliza shoo yake, ukafuata wakati wa Jux ambaye alipomaliza na kurudi nyuma ya jukwaa, Vee alimpisha mvulana huyo akae kitini kisha yeye akamkalia, jambo lililotosha kuwaaminisha watu mapenzi yao.
“Njooni muone jamani Vanessa kapakatwa na Jux tena hawana hata wasiwasi wenyewe wamejiachia kama hawapo vile, watakuwa ni wapenzi tu kwa maana huwa wanaficha sana,” alisikika akisema shabiki.
Hawakuishia hapo, kwani waliendelea kuoneshana mahaba mpaka walipoondoka katika viwanja hivyo.
Post a Comment