ATUHUMIWA KUIBA MTOTO

 


MAMA wa mtoto aliyeibwa kabla hajatimiza mwezi tangu azaliwe, Fatuma Bakari ameieleza Mahakama ya Wilaya ya Ilala jinsi mtoto huyo alivyoibwa na mshtakiwa Neema Patrick. 

Shahidi huyo na mwingine walitoa ushahidi wao jana mbele ya Hakimu Adelf Shachore kwa kuongozwa na Wakili wa Serikali, Anunciata Leopold. 

Awali mashahidi hao walikuwa watano ambao walifika mahakani kwa ajili ya kutoa ushahidi, lakini Wakili Leopold, alidai kuwa kwa mujibu wa shtaka hilo waliotakiwa kutoa ushahidi walikuwa wawili tu. 

Wakitoa ushahidi wao mashahidi hao ambao ni Fatuma Bakari na Zainabu Said, wote walikiri juu ya mtuhumiwa kufanya kitendo hicho cha kuiba mtoto. 

“Ni kweli siku ya tukio ambayo ni mwezi machi mwaka huu, mtuhumiwa alinisindikiza hospital nilipokuwa naumwa jino, kutokana na hali niliyokuwa nayo mtuhumiwa aliniomba anibebee mwanangu (Ibrahm Abdalah, ambaye hajatimiza hata mwezi) lakini mara baada ya kufika hospital maeneo ya Mbagala, Dar es Salaam, alishushuka haraka na kukimbia na mwanangu,” alidai Shahidi huyo. 

Awali mashahidi hao walitakiwa kuwa watano lakini wakili wa serikali alipinga kutoa utetezi wao, hivyo mashahidi watatu walibaki ushahidi wao utasikilizwa Juni 24 mwaka huu. 

Mtuhumiwa huyo anadaiwa kumwiba mtoto huyo maeneo ya Mbagala Machi 3 mwaka huu ambapo alikuja kukamatwa baad ya wiki mbili maeneo ya Ukonga Banana akiwa na mtoto huyo, mtuhumiwa huyo yuko nje kwa dhamana.

Kortini kwa Kumpa Mwanafunzi Mimba





MKAZI wa Mpiji Magoe Hamis Mohameid (21), amefikishwa kizimbani jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni Dar es Salaam akikabiliwa na tuhuma za kumbaka mwanafunzi (14)Jina limehifadhiwa na kumpa mimba. 

Akisomewa mashtaka mawili mbele ya Hakimu Flora Mtarania, Wakili wa Serikali Grace Lwila, alidai kuwa tukio hilo lilitokea kati ya Aprili na Mei24 mwaka huu maeneo ya huko Mpiji Magoe. 

Katika shtaka la kwanza Wakili alidai kwamba mtuhumiwa alimbaka msichana huyo kisha kumsababishia maumivu makali sehemu zake za siri. 

Wakili Lwila alidai kuwa katika shtaka la pili katika tarehe isiyojulikana maeneo ya Mpiji Magoe mtuhumiwa alimpa ujauzito mwanafunzi huyo wa kidato cha pili anayesoma shule ya Sekondari Mpiji Magoe. 

Mtuhumiwa alikana kutenda shtaka hilo na upelelezi wa shauri hilo bado unaendelea ambapo Hakimu Mtarania alisema kwamba shauri hilo linadhaminika. 

“Unatakiwa ulete wadhamini wawili walioajiriwa kutoka serikalini au katika taasisi inayotambulika kisheria watakaoweka bondi ya maandishi ya Sh. Milioni 1,” alisema Mtarania. 

Hata hivyo mtuhumiwa alirudishwa mahabusu kwa kushindwa kutimiza masharti hayo na kesi hiyo itakuja tena Juni 24, mwaka huu.

Sita wafa katika ajali, 45 wajeruhiwa Singida

 

WATU sita wamekufa na wengine 45 kujeruhiwa katika ajali mbili tofauti za barabarani zilizotokea juzi na jana mkoani Singida. 

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Singida, Thobias Sedoyeka alisema mjini hapa jana kuwa ajali ya kwanza ilitokea Juni 11 mwaka huu saa 1.30 usiku eneo la Manga nje kidogo ya mji huu kwenye Barabara Kuu ya Singida – Mwanza. 

Alisema ajali hiyo ililihusisha basi lenye usajili wa namba T174 CAV Scania la Kampuni ya Nice Line linalomilikiwa na Enock Mwita wa jijini Mwanza ambalo lilikuwa likitokea Dar es Salaam kuelekea Mwanza. 

Dereva wa basi hilo aliligonga kwa nyuma gari la mizigo lenye namba za usajili RAT 317N/ RL 0754 aina ya Benz lililokuwa limeegeshwa pembeni mwa barabara hiyo na kusababisha vifo vya abiria watatu papo hapo. Wengine wawili walifia hospitalini na kusababisha majeruhi 37. 

Kwa mujibu wa Kamanda Sedoyeka, dereva huyo ambaye alikimbilia kusikojulikana baada ya ajali kutokea, alikuwa kwenye mwendo kasi. Katika ajali nyingine iliyotokea Juni 12 saa 12.15 asubuhi katika eneo la Kindai kwenye barabara kuu ya Singida – Dodoma nje kidogo ya mji huu, gari aina ya Toyota Noah lenye namba za usajili T 998 CWG liliacha njia na kupinduka kisha kusababisha kifo cha abiria mmoja na majeruhi wanane. 

Alisema abiria wa gari hilo walikuwa wakisafiri kutoka Dar es Salaam kwenda Kahama mkoani Shinyanga kwa ajili ya kuhudhuria mazikoi ya ndugu yao na gari lao lilipofika eneo la ajali kwenye kona kali dereva wake, Paul Bundala alishindwa kulimudu kutokana mwendo kasi. 

Baadhi ya waliokufa katika ajali hiyo ni Shija Masanja,Yohana Chimole na Febronia Kway. Miili ya waliotajwa na wengine watatu ambao majina yao hayajatambuliwa imehifadhiwa katika hospitali ya mkoa wa Singida ambapo pia wamelazwa majeruhi.
-chanzo:mpekuzi

WANUSA KIFO,BODABOYA YAO YACHOMWA MOTO BAADA YA KUPORA MKOBA,SIMU

Vijana wawili wa bodaboda walikoswakoswa kuuawa baada ya kupora mkoba uliokuwa na simu wa mwanamke aliyekuwa akipita njia. Tukio hilo lilitokea Jumanne iliyopita, saa 1.30 usiku maeneo ya Sinza Afrika Sana, pembeni ya Baa ya Hongera ambapo inadaiwa ni eneo hatari kwa wizi huo.


Mmoja ya watuhumiwa akiwa hoi baada ya kupata kipigo



Shuhuda wa tukio hilo amesema kuwa tabia ya baadhi ya vijana kutumia usafiri wa bodaboda kupora watu simu na mikoba, hasa wanawake, imekua kawaida; na kwamba siku hiyo arobaini ya vijana hao ilikuwa imefika.

“Sisi tulikuwa pale baa tunakunywa, mara tukamsikia mtu akipiga kelele za mwizi…mwiziii, ile kutoka ndiyo tukawaona hawa vijana wawili wakihangaika kuwasha bodaboda yao ili wakimbie.


Askari polisi aliyeokoa maisha ya mtuhumiwa akiwa katika eneo la tukio



“Yaani ilikuwa ni Mungu tu maana bodaboda isingegoma kuwaka, tusingewapata. Basi raia wenye hasira kali wakaanza kuwashushia kipigo, aliyekuwa akiendesha pamoja na yule dada aliyeibiwa wakachukuliwa hadi Kituo cha Polisi Mabatini huku aliyekwapua akipewa kipigo,” alisema shuhuda huyo.

Hata hivyo, kijana huyo aliponea chupuchupu kuchomwa moto, kwani waliokuwa wamefuata mafuta ya petroli waliporudi walimkuta trafiki akizuia asiuawe.Kufuatia zuio hilo, raia hao walihamishia hasira zao kwenye kuichoma moto bodaboda kisha mtuhumiwa akachukuliwa hadi polisi kwa hatua zaidi za kisheria


Bodaboda iliyokuwa inatumiwa na vibaka hao ikiteketea kwa moto baada ya kuchomwa na washeria mkononi

KANYE WEST KUJITAMBULISHA KAMA MUNGU KATIKA BIBLIA ALIYOIITA "YEEZUS"





Kanye West Hujulikana sana kwa maringo yake,lakini kwa kweli Kanye West asingekufuru na kujitambulisha kama mungu katika biblia hiyo.

Kitabu hicho kitukufu kimebadilishwa na kuwa Biblia ya sasa kwa jina ''Yeezus'' na amini usiamini kila neno la Mungu katika kitabu hicho limeondolewa na badala yake msanii huyo wa muziki wa kufoka foka ameweka jina lake.

Kulingana na gazeti la The Independence nchini Uingereza,kitabu hicho kinasema kuwa katika kizazi hiki ,Kanye West ndio mkubwa na vilevile kiongozi wa kidini


Kitabu hicho kinaongezea kwamba ''katika utangulizi wetu tunamsherehekea Kanye West na vile alivyotufanyia katika maisha yetu''

Kanye West na mkewe Kim Kardashian Ijapokuwa Kanye hajatoa tamko lolote kuhusu wadhfa huo aliojipatia,amekuwa akijifananisha na Mungu hapo mbeleni.

''Mungu alinichagua mie,alinitengezea njia.Mimi ni chombo cha mungu'',alisema mwaka 2009.

''Lakini kinachoniudhi maishani mwangu ni kwamba sitawahi kujiona nikicheza muziki moja kwa moja''.,aliongezea.

Wasanii wengine waliofananishwa na Yeezy ni Marilyn Monroe na Michael Jackson. chanzo.BBC

Pesa ukiwa nazo nyingi haya ndio Matokeo ya kukufuru Kanye West moto wa jahanamu utakuhusu kesho.


Chanzo: BBC Swahili

GWAJIMA APATA DHAMANA MAHAKAMA YA KISUTU, DAR


Kiongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima leo amepata dhamana Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar atarudi mahakamani hapo Mei 4, 2015. Josephat Gwajima ameshitakiwa kwa makosa mawili kutoa lugha ya matusi na kushindwa kutunza slaha.

UZEMBE WA DAKITARI :MAHAKAMA KUU YAAMURU MGONJWA ALIPWE MIL 25...SOMA HAPA..

 

Katika hukumu nadra kutolewa nchini Tanzania, mahakama Kuu Kanda ya Tabora imeiagiza halmashauri ya wilaya ya Urambo, kulipa fidia ya shilingi milioni 25 kwa Mwamini Adam na mumewe Idrisa Jafari kutokana na madhara waliyopata baada ya uzembe uliofanywa na daktari wa hospitali ya wilaya hiyo alipokuwa akimfanyia upasuaji Mwamini.

Katika uamuzi wa shauri hilo la madai Namba 13/2011 uliotolewa hivi karibuni, Mahakama Kuu imeiagiza halmashauri hiyo kumlipa Mwamini shilingi milioni 20 kutokana na kilema alichopata kwa kuondolewa mfuko wa uzazi na kukatwa utumbo. Pia, mahakama imeiagiza halmashauri hiyo kumlipa Jafari fidia ya shilingi milioni tano ikiwa ni gharama za uendeshaji wa shauri hilo.

Akisoma hukumu, Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Tabora, Amir Mruma alikubaliana na madai ya walalamikaji kuwa madhara waliyopata kutokana na uzembe uliofanywa na Dk Jackob Kamanda ni makubwa. Jaji Mruma alisema haipingiki kwamba huo ni uzembe uliofanywa na mtumishi, hivyo mwajiri anapaswa kulipa gharama.

Aliagiza kuwa kiwango hicho cha fedha kitalipiwa riba ya asilimia saba kila siku kuanzia tarehe uamuzi ulipotolewa hadi siku mlalamikiwa atakapolipa fedha hizo.

Mwamini na mumewe walifikisha malalamiko yao Mahakama Kuu, wakidai kulipwa fidia ya shilingi milioni 505 kutokana na makosa ya uzembe uliofanywa na wataalamu wakati wa upasuaji kwa kuacha kitambaa tumboni mwa mgonjwa.

Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Wanawake, Anatory Lukonge wa Hospitali ya Itigi ambako walibaini kitambaa tumboni mwa Mwamini, aliieleza mahakama kuwa walipomfanyia upasuaji walikuta utumbo umeshikana na kizazi huku juu yake kukiwa na kitambaa.

Dk Lukonge alisema walikitoa kitambaa hicho lakini kutokana na sehemu ya kizazi kuharibika, iliwalazimu kukiondoa huku akidai kuwa hali hiyo ilisababishwa na uzembe wa daktari aliyemfanyia upasuaji

KAMA ULIPITWA NA AJALI YA GARI ILIYOUA 19 MBEYA LEO ANGALIA PICHA HAPA

Ajali za Tanzania kwenye vichwa vya habari zimezidi kuongezeka, leo April 17 2015 ajali nyingine imetokea Mbeya baada ya gari la abiria kupoteza mwelekeo na kuingia mtoni Mbeya.

Taarifa zilizothibitishwa na kamanda wa Polisi Mbeya zinasema waliofariki mpaka sasa ni 19, endelea kukaa karibu na millardayo.com kwa taarifa zaidi.





Waziri wa JK ataka shule kufanya tambiko




Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mpwapwa mkoani Dodoma wakiwa katika moja ya mikutano ya Shule 


Mpwapwa. Ingawa Serikali ya Tanzania haiamini katika ushirikina wala matambiko, kuna watu mbalimbali na jamii tofauti zinaamini katika mambo hayo.

Serikali imekuwa ikipinga na kulaani vitendo vinavyoashiria ushirikina hata kuwashughulikia watu wanaonaswa wakishabikia imani hizo potofu.

Hata hivyo baadhi ya maeneo nchini bado watu wake wanaendeleza imani za kishirikina pamoja na matambiko.

Hata hivyo siyo jambo la kawaida kwa kiongozi hasa wa Serikali kusikika akihimiza kufanyika kwa matambiko ingawa kimsingi tukio hilo linahesabiwa kuwa ni namna ya kutafuta ufumbuzi kwa njia za kiakili na siyo ushirikina.
Ndivyo ilivyotokea hivi karibuni wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma.

Ni kama hadithi, lakini katika tukio la Februari 8 asubuhi, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alitoa maagizo ya kufanyika kwa tambiko muda mfupi baada ya kuwasili eneo la Sekondari ya Mpwapwa kwa ajili ya kutoa pole na kuwafariji wanafunzi wa kike ambao bweni lao liliteketea kwa moto.

Baada ya maelezo kutoka kwa mkuu wa shule hiyo pamoja na mbunge wa Jimbo la Mpwapwa Gregory Teu, naibu waziri aligeuka na kutoa maagizo ya kufanya matambiko mazito katika eneo hilo.

Ilivyokuwa

Mkuu wa Sekondari ya Mpwapwa, Nelson Milanzi alianza kwa kutoa simulizi ya tukio la moto ulioteketeza mabweni ambalo lilitokea Januari 20 mwaka huu akisema kuwa vituko vilianza siku moja kabla ya tukio.

“Wanafunzi walitoa maelezo kwamba kulikuwa na nyoka mkubwa aliyeonekana akishuka kutoka katika paa la bweni na alipodondoka chini, uliwaka moto mkubwa. Lakini cha ajabu, moto huo uliunguza shuka mbili za bluu mashati mawili na ghafla ulizimika. Majivu niliyakuta,” anasimulia Milanzi.

Mkuu huyo anasema kuwa tukio hilo lilikuwa na ajabu kiasi cha kumfanya akusanye wanafunzi wa kiume na walimu zaidi ya 10 na kuwapandisha katika dari na kuanza kufanya msako mkali, lakini hawakumuona nyoka huyo.

Siku iliyofuata, mambo yaligeuka, nyoka yule yule aliyeungua jana, alitua chini ghafla na safari hii kukiwa na mwanafunzi mmoja wa kike na moto uliwaka na kushika kasi ya ajabu, ambapo kila kilichokuwa ndani kiliteketea.
CHANZO:MWANANCHI

MAJANAGA: MAPACHA WAPENDANA ,WALIONA WAUNGANE PIA KWENYE NDOA MOJA..

  

image52Tumezoea kuona pacha wengi wakishare mambo wanayopenda kwa pamoja, kitu kama aina ya mavazi wanayovaa na vinginevyo, iliwahi kutokea story ya mapacha walioolewa na pacha wenzao Tanga.
Kutoka Afrika Kusini mapacha wawili wanawake, Owami na Olwethu wenye umri wa miaka 26 wameingia kwenye headline kutokana na kukubaliana kuolewa na mwanaume mmoja, Mzukiseni Mzazi ambapo mapacha hao wamesema walikuwa wakishirikiana kwa mambo mengi  tangu wakiwa wadogo huku wakiwa na ndoto ya kuolewa na mwanaume mmoja.
South-African-twin-sisters-who-married-the-same-man1

LAANA! AIBU KUBWA! MUUZA GENGE ACHEZEA KICHAPO KWA KUNASWA NA MKE WA MTU

Aibu kubwa! Muuza genge mmoja kwenye Soko la Mji Mpya mjini hapa ambaye jina halikupatikana mara moja, amejikuta akichezea kichapo kwa madai ya kunaswa na mke wa mtu kisha kutembezwa mtupu mtaani.
Muuza genge aliyechezea kichapo baada ya kunaswa na mke wa mtu na kutembezwa mtupu mtaani.

Fumanizi hilo lililojaza umati wa jinsi na rika zote wakiwemo watoto lilijiri katikati ya wiki hii, maeneo ya Mji Mpya ndani ya chumba na kitanda cha wanandoa hao. 
Kikiwa kwenye mishe zake, kile kikosi kazi cha Oparesheni Fichua Maovu (OFM) cha Global Publishers mkoani hapa kilipenyezewa kuwepo kwa ‘uovu’ huo ambapo hakikulaza damu.

ENEO LA TUKIO
OFM, ikiwa eneo la tukio ilijikusanyia madai mazito juu ya jamaa huyo kuwa amekuwa na kasumba ya kumhonga vyakula mke huyo wa mtu ambaye naye kwa kukosa uaminifu kwenye ndoa alijikuta akiingia mkenge hasa mumewe anapokuwa safarini kwa kuwa ni mtu wa kusafiri katika biashara zake binafsi.
Ilidaiwa kwamba, mwanamke huyo hutumia mwanya huo kumwingiza mchepuko wake huyo kwenye chumba na kitanda anacholala na mumewe kisha ‘kufanya yao’.

Baada ya kukolea huku mahaba niue yakitajwa na sauti ‘tamutamu’ zikisikika chumbani, majirani walikerwa na kitendo hicho cha jirani yao kudhulumiwa ‘mali’ zake ndipo wakaamua kumpa ‘ubuyu’ mume.
Ilisemekana kwamba, mume, akishirikiana na majirani aliowaomba ushirikiano, aliweka mtego ambapo alijifanya anasafiri kama kawaida.

Wananchi wakimshuhudia muuza genge huyo akihadhirika baada ya fumanizi.

Siku ya tukio, saa husika ilifika, kama kawaida jamaa alifika nyumbani kwa wanandoa hao kisha kuchoma chumbani kwa wanandoa tayari kwa kulicheza ‘segere’.

LAIVU NA SUTI YA KUZALIWA
Mwenye mke, akiwa chimbo alitonywa na majirani kuwa mambo ‘yamekwiva’ chumbani ndipo akawaibukia na kumkuta jamaa laivu akiwa mtupu. Haikujulikana kama ilikuwa ‘tayari au bado’.
Akiwa na hasira, mwenye mke alidaiwa kumshushia kipigo mgoni kilichomfanya kuloa damu chapachapa na baadaye kumtoa nje akiwa mtupu kisha kumtembeza mtaani kwenda nyumbani kwake huku ‘kadamnasi’ ikipiga kelele ‘watu weweee...”

Katika hali ya kushangaza, mwenye mke aliomba mkewe asipigwe picha akidai bado anampenda na hayuko tayari kumuacha. 
Kwa upande wake, jamaa huyo aliyedaiwa kufumaniwa alipohojiwa na OFM, aligoma kuzungumza na badala yake alificha uso kwa aibu.

MAJANGA: WANASWA WAKIFANYA MAPENZI KITUO CHA POLISI


AMA kweli binadamu siyo waoga! Watu wawili ambao majina yao hayakupatikana mara moja, waliamua kujitoa fahamu na kuamua kufanya mapenzi ndani ya gari nje ya Kituo cha Polisi cha Alimaua kilichopo Kata ya Kijitonyama jijini Dar, OFM wanakumegea mkanda mzima.


Watu hao wakiendelea kufanya mambo yao.

Tukio hilo la aina yake lilinaswa saa nane usiku wa Jumatano wakati kikosi kazi cha Oparesheni Fichua Maovu (OFM) kikiwa kazini kusaka matukio mbalimbali ya usiku mnene.
Ilikuwaje?

Awali, baadhi ya watu waliokuwa wakitoka kuangalia mechi ya Kombe la Capital One kati ya Chelsea na Liverpool nchini Uingereza waliwaona wawili hao wakipaki gari eneo hilo la polisi kana kwamba walikuwa na shida muhimu ya kiusalama kama si kisheria. Kituo hicho kilikuwa kimefungwa!

Tofauti na matarajio ya mashuhuda hao, gari hilo aina ya Toyota Mark II (namba za usajili tunazo) lilizimwa taa za ndani na kuachwa ikiunguruma kisha watu hao ambao haikufahamika kama ni wapenzi au ni changudoa na mteja wake walianza kushikana kimahaba.

DEREVA ALALIA USUKANI

OFM walizidi kuambiwa kuwa, mashuhuda walijiongeza na kubaini kwamba wawili hao walikodi gari hilo kwani walipoanza kushikana, dereva aliegemea usukani kwa hali iliyotafsirika kuwa, alikuwa akiwapa nafasi abiria wake wamalize ‘mambo’ yao.
He! Mchezo wAnoga

Muonekano wa kituo hicho.

“Unaweza kusema wawili hao walikuwa ndani ya fensi nyumbani kwao, kwani wanazidi kufanyiana mambo ya chumbani. Hivi hapa sisi tunawashangaa,” shuhuda mmoja aliwaambia OFM.


OFM WATINGA

Ndani ya dakika chache, makamanda wa OFM wanaopatikana kwa saa 24, walikuwa wamewasili eneo la tukio kwa kutumia pikipiki zao maalum ziendazo kasi.
Kitendo bila kuchelewa, zoezi la kuwafotoa picha kwa mbali lilianza na ndipo waliposhituliwa na mwanga wa ‘flash’, hali iliyomfanya dereva wa gari hilo kutaka kuondoa gari.

WATAITIWA, WAKUTWA CHAKARI
Kwa kutumia ujasiri wa hali ya juu, makamanda hao kwa kusaidiana na mmoja wa mashuhuda anayeishi eneo hilo walilizuia gari lisiondoke na ndipo ilipobainika kuwa, licha ya kunaswa wakiibanjua amri ya sita ya Muumba pia watu hao walikuwa chakari kwa pombe.

WASHINDWA KUJIBU MASWALI
Hata hivyo, kutokana na kuwa tilalila, ilikuwa vigumu kuwahoji kwani kila walipoulizwa kwa nini waliamua ‘kupumzikia’ nje ya kituo hicho cha polisi, waliishia kuinamisha vichwa.


OFM YAMTOA NDUKI DEREVA
Mazingira hayo yaliwalazimu makamanda wa OFM kumwamuru dereva ambaye alikuwa akijitambua kuliondoa gari hilo kituoni hapo kabla msala mkubwa haujawapata.
Zote hizo pombe

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camillius Wambura.

Uchunguzi uliofanywa na OFM umebaini kuwa, kitendo cha watu hao kupaki gari eneo la kituo cha polisi na kufanya uzinzi kilitokana na pombe walizokuwa wamekunywa hivyo akili yao iliwatuma kuwa lile lilikuwa eneo salama zaidi kwao.

OFM WAMSAKA KAMANDA WA POLISI
Ili kutaka kujua ni kwa nini kituo hicho cha polisi kilipigwa ‘loki’ wakati usiku ndiyo matukio ya uhalifu yako kwa wingi, OFM walimwendea hewani Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camillius Wambura.
OFM: “Afande, habari?”
Wambura: “Nzuri.”

OFM: “Naongea na RPC wa Kinondoni?”
Wambura: “Unasemaje?”

OFM: “Mimi ni mwandishi napiga simu kutoka Global Publishers...”
Wambura: “Nipo kwenye mkutano. Nenda ofisini (Oysterbay Polisi) utamkuta mhusika.”
OFM: “Naomba unisaidie pale nitamkuta nani? Au namba yake ya simu.”

Wambura: “Ifike mahali sasa, waandishi muwe mnafika ofisini kwa taarifa kama hizi (za kiofisi). Nitajuaje kama wewe ni mwandishi? Nenda pale utaoneshwa kaimu kamanda uzungumze naye.”
OFM OYSTERBAY POLISI
OFM walifunga safari hadi Kituo cha Polisi Oysterbay jijini Dar na kumuulizia kaimu kamanda wa mkoa lakini afande aliyekuwa mapokezi alisema ametoka kikazi nje ya kituo.

HII DUNUNIA INAMAMBO!! BINTI ALAZIMISHA KUFANYA MAPENZI NA WATOTO

 
UKISTAAJABU ya Musa utayaona ya Firahuni! Binti aliyefahamika kwa jina moja la Afsa (14), anayesoma darasa la 7, ametiwa nguvuni na jeshi la polisi akidaiwa kuwafanyia ukatili na kuwadhalilisha watoto wawili wa kiume (majina kapuni) wa mama yake mkubwa kwa kuwakang’ata nyeti zao akiwalazimisha kufanya nao mapenzi.

Binti anayefahamika kwa jina moja la Afsa (14) anayetuhumiwa kuwanyanyasa watoto wadogo.

Tukio hilo la kushangaza ambalo lilijaza umati wa watu , lilitokea wiki iliyopita katika mtaa wa Nyerere, Kata ya Mafisa, mkoani hapa.
Kamanda wa OFM, Mkoa wa Morogoro akiwa kazini, alipokea taarifa kutoka kwa wananchi wa mtaa huo wakimuomba afike fasta.
Bila kuchelewa kamanda alitia timu na kukutana na akina mama wawili ambao walishusha ‘vesi’ za tukio hilo:

Binti huyo akiwa chini ya ulinzi, wa pili kulia ni mmoja wa watoto walionyanyaswa na binti huyo.

“Sisi ni wakazi wa mtaa huu wa Nyerere ambao tunaishi na Mama Mese mwenye watoto wawili wa kiume, anaishi pia na mtoto wa mdogo wake (Afsa) aliyempa jukumu la kuwalea wanaye.
“Cha kushangaza Afsa amekuwa akiwafanyia ukaliti wa kutisha watoto hao. Leo amewatoboa macho na njiti ya viberiti kuwapiga mateke na kuwasukumiza ukutani, mbaya zaidi aliwang’ata nyeti zao alipokuwa akiwalazimisha kuduu nao.

Makamanda wa Polisi wakimchukua mtoto mwingine aliyenyanyaswa na binti mtuhumiwa.

“Kama majirani tumemuuliza mama Mese inakuwaje wanaye wanateswa kila siku na yeye hachukui hatua yoyote, akasema hataki kwenda polisi wala kwa mwenyekiti wa mtaa anaogopa mtoto wa mdogo wake atafungwa sasa sisi tumeamua kukuita uje kushudia tukio hili bichi,” walisema kina mama hao walioomba hifadhi ya majina.

Mwanahabari wetu alifika kwenye nyumba hiyo na kumkuta mama Mese akiwa na watoto wake hao wakiwa na makovu mwili mzima, alipoulizwa undani wa tukio hilo na kwa nini hatoi taarifa katika vyombo vya usalama? Alifunguka:

Binti anayetuhumiwa akichukuliwa kwenye pikipiki kwenda kituo cha Polisi.


“Mimi ni mfanyakazi pia mwanafunzi, nasoma chuo hivyo wanangu hulelewa na Afsa ambaye ni mtoto wa mdogo wangu. Kweli wanangu wamepigwa na kufanyiwa ukatili na huyu mtoto wa mdogo wangu lakini suala hili sitaki lifike popote, nimepanga kumrudisha kwao Moshi,” alisema Mama Mese.
Katika hali ya kushanga, paparazi wetu alipotaka kumhojia Afsa, mama huyo alikataa jambo lililowakera majirani na kuibua vurugu.

Baada ya vurugu kuwa kubwa, jirani mmoja aliwatonya polisi ambao walifika ndani ya muda mfupi na kufanikiwa kumkamata Afsa kumpeleka kituoni kwa ajili ya hatua za kisheria huku mjumbe wa serikali ya mtaa huo, Yusuf Juma akishuhudia tukio hilo na kulilaani.

AAMUA KUINGIA NA SHELA LA HARUSI MITAANI...KISA NI WAZAZI WAKE!


Mwanamke mmoja nchini Misri ameamua kukatiza na gauni la arusi mitaani kupinga masimango anayokutana nayo kwa kuchelewa kuolewa.

Samah Hamdi mwenye miaka 27 alifikia uamuzi huo baada ya kuchoshwa na kashfa kutoka kwa watu wanaomzunguka ikiwemo familia yake hasa mama yake mzazi ambao wamekua wakimsema kutokana na kutokua na mume mpaka sasa.

Hamdi ambaye ni mwanafunzi wa shahada ya uzamili alisema ameamua kutembea hivyo mitaani na kamwe hawezi kuacha dhamira yake hiyo ikiwa kama ishara ya kupinga mila na desturi inayowakandamiza wanawake wasioolewa.

Samah Hamdi akiwa anatafakari jambo huku akiwa amevaa gauni lake la harusi katika moja ya mitaa jijini Cairo

TUHUMA NZITO: RUSHWA YA NGONO YAMNASA MFANYA BIASHARA

 
 
Hii ni tuhuma nzito! Katika hali inayoonesha maadili Bongo yanagaragazwa kwa kiwango cha kutisha, mapema wiki hii jamaa mmoja mfanyabiashara mwenye asili ya Kihindi almaarufu Kanjibai au Ponjoro, alinaswa kitandani akiwa mtupu na mwanamke aitwaye Hidaya ambaye ni mke wa mtu, akidaiwa kudai rushwa ya ngono ili ampe ajira.

Kanjibai akiwa mpole baada ya kufumaniwa.

OFM YATONYWA
Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers, ikiwa kwenye ‘mingo’ zake ilipewa ‘ubuyu’ na vyanzo vyake kwamba ifike katika nyumba moja iliyopo Tandale jijini Dar es Salaam kwani kulikuwa na zoezi la ufichuaji wa maovu.

MAOMBI YA KAZI
Kabla ya tukio hilo, ilidaiwa kwamba hivi karibuni Kanjibai na Hidaya walikutana maeneo ya Kariakoo jijini Dar ambapo mwanamke huyo alikwenda kutafuta kazi.
Ilidaiwa kuwa baada ya kusalimiana mazungumzo mengine yaliendelea huku jamaa huyo akitaka mambo matamu-matamu ya chumbani kwa ahadi ya ajira:
“Kazi kwishapata lakini lete ile kachori (rushwa ya ngono), mimi patia kazi wewe, sawasawa?”

 
KANJIBAI ATUMA VIMESEJI VITAMU
Ilidaiwa kwamba baada ya wawili hao kuagana, Kanjibai alianza kumchombeza Hidaya kwa ‘vijimeseji’ vitamu-vitamu kupitia mitandao ya simu za mkononi hasa hizi za kisasa za kuteleza ‘smart phones’.
Iliendelea kudaiwa kwamba siku ya siku, wakiwa nyumbani kwao maeneo hayo ya Tandale, Dar, mume wa Hidaya aligundua mchezo huo mchafu baada ya kunasa mawasiliano haramu kati ya Kanjibai na mkewe ambapo alianza kumbana ‘maiwaifu’ wake ampe ushirikiano wamshike ugoni.

UTETEZI
Ilidaiwa kwamba, katika utetezi wake, mwanamke huyo alimwambia mumewe kuwa jamaa huyo alikuwa akitaka mapenzi ili ampatie ajira kwenye kampuni moja iliyopo Kariakoo, Dar.

MTEGO WAANDALIWA
Baada ya kukubaliana, mume na mke waliandaa mtego ambapo Hidaya alimwelekeza Kanjibai anakoishi Tandale.Ilielezwa kwamba, Kanjibai, bila kujua kinachoendelea huku akiomba maelekezo katika kila hatua, alifanikiwa kufika kwa wanandoa hao na kuzama ndani.Ikasemekana kwamba, jamaa huyo alipotimba ndani alikaribishwa chumbani ambapo hakuchukua muda, akasaula nguo zote na kubaki mtupu akiwa tayari kutekeleza uzinzi.


BONGE LA FUMANIZI
Baada ya Hidaya kutoa ishara kwa mumewe kuwa mambo ‘yameiva’, OFM wakatonywa ambapo bila kuchelewa, kama kawaida yake, mkuu wa zamu aliwaagiza vijana wake ambao walitoka mkuku kwa kutumia pikipiki ziendazo kasi kuelekea eneo la tukio.

OFM ilipofika eneo la tukio ilikuta bonge la sekeseke la fumanizi likiendelea huku Kanjibai akiwa mtupu kitandani, chumbani kwa wanandoa hao akiomba msamaha kwa kutumia Kiswahili cha ‘makabachori’ huku akiahidi kutorudia mchezo huo mchafu.

KISWAHILI MBOVUMBOVU
“Iko samehe mimi bana, pana jua hii kama mke ya mtu, iko najua ishi peke yake, hapana ambiya mimi kama olewa, samehe mimi ngoja ita kaka yangu jua vizuri Kiswahili ongea na wewe lakini hapana peleka mimi polisi, iko ogopa sana pelekwa Segerea,” alisikika Kanjibai akijitetea huku akimuomba mume wa mwanamke huyo pamoja na ndugu zake wamsamehe na wasimpeleke polisi kwani anaogopa kupelekwa Gereza la Segerea jijini Dar.

MKONO WA SHERIA
Hadi OFM inaanua virago eneo la tukio, mume, mke na wapambe walikuwa katika taratibu za kufuata hatua zinazostahili ili kumfikisha Kanjibai kwenye mkono wa sheria.

ONYO
Gazeti hili linatoa onyo kwa vitendo viovu vya ngono na kushauri wote wanaohitaji wenza kufuata taratibu zinazostahili ili kupunguza kasi ya mafumanizi, maradhi na migogoro mbalimbali katika jamii la sivyo OFM ipo kazini kila sehemu, kila saa kuwaumbua. - Mhariri.

MAJANGA: IKIDHIBITIKA ROSE MHANDO AMETOA MIMBA YA MIEZI 7 ATAENDA JELA MIAKA 7


Stori: Waandishi Wetu/Risasi Mchanganyiko KITENDO cha mwimbaji nyota wa muziki wa Injili, Rose Muhando (pichani) kudaiwa kutoa mimba yenye umri wa miezi saba, endapo kitathibitishwa na mamlaka zinazohusika, kinaweza kusababisha kupewa adhabu ya kifungo cha miaka 7 jela, Risasi Jumatano lina mkanda kamili.

Mwimbaji nyota wa muziki wa Injili, Rose Muhando akiimba wakati akiwa mjamzito. 

Mwishoni mwa wiki iliyopita, ilidaiwa kuwa Rose, mwimbaji mwenye maskani yake mjini Dodoma, alikuwa ameitoa mimba aliyokuwa nayo, ambayo anadaiwa kupewa na mcheza shoo wake. Kama ingeenda salama na kujifungua, ingempatia mtoto wake wa nne. 

Kufuatia madai hayo, gazeti hili lilifanya mawasiliano na wadau kadhaa, miongoni mwao wakiwa ni wanasheria, wanamuziki wenzake na viongozi juu ya ishu hiyo iliyoushtua ulimwengu wa Injili. Mwanasheria mmoja maarufu nchini, ambaye aliomba hifadhi ya jina lake kwa sababu alizodai ni za kimaslahi, alisema kutoa mimba ni kosa kisheria na wahusika, akiwemo mama na daktari aliyeshiriki kukamilisha tukio hilo, wanapaswa kushtakiwa na kuhukumiwa. 

“Inategemea, kama alitoa mimba kwa sababu za kimatibabu, yaani ili afya yake iwe sawa ni lazima atoe ujauzito alionao, hilo siyo kosa, lakini kama alitoa kwa sababu nyinginezo nje ya hapo, ni kosa la jinai linalostahili adhabu.

Rose Muhando. 

“Kwa mujibu wa Sheria za Kanuni ya Adhabu sura ya 16, kifungu cha 150, daktari anayehusika na kosa hilo adhabu yake ni kifungo cha miaka 14 jela na mama aliyetolewa ujauzito huo, kwa mujibu wa kifungu cha 151, anastahili kifungo cha miaka saba jela,” alisema mwanasheria huyo. 

Kuhusu sababu za kumfunga kwa miaka mingi daktari badala ya mama aliyetaka kutolewa, ‘lawyer’ huyo alisema hii inatokana na kiapo ambacho madaktari huapa ambacho kinawataka kulinda uhai wa mtu na pia ni kukiuka maadili ya kazi yao. 

“Mahakama itakuwa kali zaidi kwa madaktari kwa sababu ya dhamana ya kiapo chao. Huu unakuwa ni mfano kwa madaktari wengine ili wasimamie maadili na viapo vyao,” alisema mwanasheria huyo. Katibu wa Chama Cha waimba Injili, Stella Joel, alipoulizwa kuhusu maoni yake juu ya kadhia hiyo, alisema chama chao hakina taarifa za tukio hilo, lakini wanaweza kuchukua hatua kama Polisi watalifanyia kazi jambo hilo kwa vile ni kosa la kijinai. 

“Kutoa mimba ni kosa la Jinai, kwa hiyo kama Polisi watalifanyia kazi, sisi tutatoa tamko na kuchukua hatua, kwa sasa hatuna la kufanya, tunasikia katika vyombo vya habari na mitandao, tukimuuliza anakataa,” alisema. 

Waimbaji wenzake, Bahati Bukuku na Christina Shusho walionyesha kushangazwa na tukio hilo, wakidai limewashtua na halikutarajiwa. “Rose ni mtu mzima, kama kweli tukio hili lipo, basi huo ni uamuzi wake na Mungu wake, inategemea na mapatano yao, kila mtu ana maamuzi yake ila nimeshtushwa sana,” alisema Bahati Bukuku. Shusho alisema jambo hilo ni baya na kosa kisheria, lakini hata hivyo ni suala binafsi linalomhusu mhusika.Rose Mhando mwenyewe alitafutwa katika simu yake ya mkononi ili kusikia kauli yake juu ya suala hilo, lakini zaidi ya mara nne, simu yake iliita hadi kukatika pasipo kupokelewa. 

CHANZO: GPL

KITUO CHA POLISI IKWIRIRI CHAVAMIWA NA MAJAMBAZI, ASKARI WAWILI WAUWAWA

 



Mfano wa bunduki aina ya SMG zilizoibiwa.

Mfano wa bunduki aina ya SAR zilizoibiwa na majambazi.

Mfano wa bunduki aina ya Shotgun iliyoibiwa na majambazi.

MAJAMBAZI yaliyojihamu kwa silaha yamevamia Kituo cha Polisi cha Ikwiriri, Rufiji mkoani Pwani na kuua askari wawili na kupora silaha zilizokuwepo kituoni hapo.

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo, huku askari wanaodaiwa kupotenza maisha ni Cop. Edgar aliyekatwa mapanga na WP Judith aliyepigwa risasi ubavuni upande wa kulia na kutokea upande wa kushoto.

Hivi sasa hali ni tete katika eneo hilo na watu wamekusanyika huku polisi wakiongeza nguvu kusaka wauaji katika tukio la uvamizi, kituo cha polisi Ikwiriri, Rufiji, Pwani.

Silaha zilizoporwa ni SMG 2, SAR 2, SHORTGUN 1, silaha 2 za mabomu ya machozi na risasi 60 za SMG.

MAJANGA: MBARONI KWA MAPENZI YA JINSIA MOJA

DUNIA imekwisha! Wasichana wawili warembo, Maua Sadick (24), mkazi wa Stakishari, Ukonga wilayani Ilala na Lucy Fred (23), mkazi wa Karakata jijini Dar es Salaam, wanashikiliwa katika Kituo cha Polisi Stakishari, Ukonga, Dar kwa kesi yenye jalada STK/RB/463/2015 wakidaiwa kufanya mapenzi ya jinsia moja. 

Warembo, Maua Sadick (mwenye shati la draft) na Lucy Fred wakipozi kimahaba. 

Warembo hao walikamatwa Januari 12, mwaka huu saa sita mchana, nyumbani kwa Maua wakidaiwa kufanya ngono kinyume cha sheria ya kujamiiana ambapo watu wa jinsia moja ni makosa kukutana kimwili. 

NDUGU, MAJIRANI WAKERWA 
Kwa mujibu wa habari za kipolisi, kukamatwa kwa Maua kulitokana na taarifa za baadhi ya ndugu na majirani zilizopelekwa polisi kwamba, wasichana hao wanapokuwa kwenye tendo la ndoa wamekuwa wakipiga kelele za udhalilishaji kwa familia zao. 

Wasichana hao wakiwa maeneo tofauti. 

WALISHAONYWA, HAWAKUSIKIA
Vyanzo makini kutoka jirani na makazi ya Maua vinadai kuwa, kutokana na hali hiyo, baadhi ya watu walijitolea kuwaonya wasichana hao kuwa na staha wawapo kwenye faragha yao lakini pia wao ni wanawake haiwezekani wacheze mchezo huo wenyewe kwa wenyewe lakini hawakutaka kusikia. 

MAJIRANI WAFUNGULIA REDIO SAUTI YA JUU
“Ilifika mahali wakiingia chumbani kuanza mambo yao sisi majirani tunazidisha sauti za redio ili watoto wasisikie lakini na wao sauti zao zinakuwa juu kushinda za redio,” alisema jirani mmoja akiomba jina lake lifichwe ili kukwepa uhasama. 

Alisema kutokana na hali hiyo waliamua kufikisha habari hizo polisi kwani ni kinyume cha sheria watu wa jinsia mmoja kukutana kimapenzi. 

Mrembo Lucy Fred ambaye ni mpenzi wa Maua Sadick.


HISTORIA YA LUCY
Wakizidi kuzungumza na Uwazi, majirani hao walisema, Lucy ambaye ndiye anaitwa mke na Maua amekuwa akitoka nyumbani kwa wazazi wake Karakata kwa lengo la kumfuata Maua. 

SIKU YA TUKIO
Ilisemekana kuwa, siku ya tukio, majirani walipoanza kusikia ‘zile sauti zao’, waliwapa polisi namba ya simu ya mtu wa jirani na Maua kwa lengo la kusaidia kufika nyumbani hapo. 

“Polisi walipofika waligonga mlango kwa muda mrefu bila kufunguliwa na kelele za mahaba zilizidi kusikika. Baadaye, nadhani wakati wanapumzika sasa, Maua alifungua mlango mkubwa na kukutana na macho ya polisi, wakambana na kumtaka waende wote alipo Lucy, wakaenda chumbani na kumkuta.
“Pia polisi walikuta kidude ambacho huwashwa kwa betri kilichodaiwa pia hutumika wakati wa tendo,” kilisema chanzo. 

Warembo hao kama wanavyoonekana kwenye picha zao za instagram. 

HISTORIA YA MAUA
Maua ni binti ambaye ni yatima, amekuwa akiishi mwenyewe kwenye nyumba hiyo kubwa ya familia hivyo kumwita Lucy mara kwa mara kwa madai ya kufanya ufuska huo kwa vile wana uhuru.
Inasemekana kuwa, Maua siku zote amekuwa akivaa mavazi ya kiume licha ya kwamba, ni mwanamke kamili. 

POLISI WASHANGAA
Taarifa kutoka vyanzo vya ndani ya jeshi la polisi zinadai kwamba, hata wakiwa mahabusu ya kituo hicho, wawili hao wamekuwa wakioneshana mapenzi baina yao kitendo kilichowashangaza mahabusu wengine na polisi pia. 

Uwazi lilifika nyumbani kwa Maua na kukutana na mdogo wake aitwaye Aziz ambaye alikiri kukamatwa kwa Maua na kwamba tangu akamatwe hajarudi na wala hajui kinachoendelea huku akisema asingependa kuzungumzia suala hilo kwa sababu ya kutupiwa lawama na wanandugu kwamba yeye ndiye aliyepeleka taarifa polisi. 

Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Ilala, SACP Mary Nzuki.


“Mimi sikai hapa, nimefika hivi karibuni nikitokea mkoani. Ndugu wananituhumu mimi kuita polisi, sijui mtu aliyewapa askari namba yangu wakanipigia kama wageni wanaokuja nyumbani, nikawapa ramani na walipofika ndipo nikagundua ni askari,” alisema Aziz. 

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa, George Mtambalike alipohojiwa na gazeti hili ofisini kwake alithibitisha kukamatwa kwa wasichana hao kwa madai ya kufanya mapenzi ya jinsia moja na aliwatembelea Kituo cha Polisi cha Stakishari. 

Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Ilala, SACP Mary Nzuki alikiri kukamatwa kwao na akasema uchunguzi unaendelea.
-CHANZO:GPB

MATUKIO KIBAO YA UJAMBAZI BENKI, HATARI KUBWA!


WAKATI kukiwa na dhana ya baadhi ya wafanyakazi na wateja wa mabenki nchini kuvujisha taarifa za wateja wanaotoa kiasi kikubwa cha fedha kwa majambazi ambapo mwishowe wateja hao huvamiwa na kuporwa, Oparesheni Fichua Maovu (OFM) imetinga ndani ya benki kadhaa jijini Dar na kugundua udhaifu mkubwa katika ulinzi, Ijumaa Wikienda limeshika ushahidi mkononi.

Makamanda wa OFM(katikati) wakiwa ndani ya benki.

Kutokana na matukio mfululizo ya wateja kuvamiwa mara baada ya kutoka kuchukua fedha ndani ya mabenki, watu kadhaa walitoa malalamiko yao kwa OFM wakitaka suala hilo lifanyiwe kazi kwa kuwa wao wanaamini kuna udhaifu mkubwa kwenye sekta ya ulinzi.

Wakizungumza na Ijumaa Wikienda kwa masharti ya kutotaja majina yao, baadhi ya watu hao walisema wapo wafanyakazi au wateja ambao wanaweza kuingia benki na kutoa taarifa za mteja mwingine ambaye anatoa pesa nyingi kwani ulinzi ni mdogo.

MALALAMIKO
“Unajua ukikuta mtu anaweza kuingia benki akaongea na simu akiwa kwenye foleni ni tatizo. Siku hizi hata baadhi ya mabenki, hata wale wanaotoa huduma (teller) nao wana uwezo wa kuwasiliana kwa simu huku kukiwa na wateja na wao wakiwa kwenye madirisha yao.

“Tabia hii ndiyo chanzo cha ujambazi mkubwa unaotokea siku hizi. Mtoa huduma anaweza kumwambia jambazi nje kwa simu kwamba kuna mtu amevaa suti anatoka na mkoba mweusi una milioni kumi kwa sababu yeye si ndiye amemtolea?
“Au wateja wanaoongea na simu wakiwa kwenye foleni, ni rahisi kuvujisha taarifa kwa majambazi. Unajikuta unakwenda kuvamiwa mbele ya safari kumbe watu walikufuatilia tangu ndani ya benki,” alisema mmoja wa watu hao.

Mmoja wa makamanda wa OFM akiongea na simu bila kizuizi chochote kutoka kwa walinzi wa benki.

OFM YAINGIA KAZINI
Baada ya kupokea malalamiko hayo, OFM ilijipanga na kuanza kuzungukia benki mbalimbali jijini Dar ili kupata ukweli.

KAZI YAANZA
Januari 12, mwaka huu, saa 7:24 mchana, makamanda wa OFM walitinga ndani ya benki moja kubwa iliyopo maeneo ya Mnazi Mmoja, Dar, mmoja akiwa na bastola kibindoni huku mwingine akiwa na simu ya mkononi ambayo aliitumia kuongea na watu kila mara bila kuchukuliwa hatua yoyote licha ya kuwepo kwa matangazo yaliyosomeka; switch off your phone (zima simu yako).

Kama hiyo haitoshi, makamanda waliokuwa na kibarua cha kuchukua picha ya kile kilichokuwa kikiendelea ndani ya benki hiyo, walishuhudia wateja wengine wakizungumza kwa simu kwa sauti za juu huku wenzao wakitoa fedha bila kuhofia usalama wao.

SAA 7: 43 MCHANA
Bila kutambulika, kamanda mmoja wa OFM alichukua simu yake ya mkononi na kumpigia mwenzake aliyekuwa nje na kuzungumza naye kwa sekunde 33 kisha kukata na kupiga tena ambapo alitumia sekunde 17 na kuendelea kuchati na watu wengine bila kizuizi chochote.
Kamanda mwingine aliyekuwa na bastola ndani ya mfuko alijaza fomu ya kuweka fedha (deposit slip) na kwenda moja kwa moja kwa ‘teller’ kuweka fedha zake.

Kamanda wa OFM akiwa na bastola ndani ya benki.

Hadi saa 8:02, makamanda wanaondoka kwenye benki hiyo, hakuna mhusika hata mmoja aliyeshtukia zoezi hilo, jambo lililoonesha kuwa uvamizi ndani ya benki au kuvuja kwa taarifa za wateja wanaohudumiwa ni rahisi kuliko inavyoweza kudhaniwa.

BENKI YA PILI
Januari 17, mwaka huu, saa 5:16 asubuhi. makamanda wa OFM walitinga ndani ya benki nyingine iliyopo maeneo ya Mwenge jijini Dar, zoezi likiwa kama lile la awali ambapo kamanda mmoja wa OFM alibeba bastola na kujitoma nayo ndani huku mwingine akiwa na simu ya mkononi.

Saa 5:17, kamanda wa OFM akiwa na bastola inayoonekana kuchomoza nje ya mfuko wa suruali, aliingia ndani ya benki hiyo na kujaza fomu bila kumjali mlinzi aliyekuwa pembeni.
Saa 5:19, kamanda akaelekea upande wa maulizo ambapo aliomba maelekezo ya jinsi ya kufungua akaunti na kuambiwa asubiri kwa muda.

Dakika 7 baadaye, mhudumu wa maulizo alimwita kamanda na kumpa fomu yenye maelezo ya jinsi ya kufungua akaunti na kuondoka zake.
Saa 5:21 kamanda aliyekuwa na simu alimpigia mtu aliyekuwepo nje ya benki na kuongea naye kwa dakika 2 huku hali ikiwa kama ile ya benki ya awali ambapo hakukuwa na katazo lolote kutoka kwa mlinzi wa benki hiyo.
Timu nzima ya OFM iliondoka maeneo hayo kwa mtindo wa kijasusi bila kushtukiwa jambo ambalo kwa benki iliyojizatiti kwa ulinzi, makamanda wa OFM wangeshtukiwa mapema.

Kamanda Kova akizungumza jambo.

LENGO LA OFM
Lengo la OFM kufanya ushushu kuhusu madai ya udhaifu wa ulinzi kwenye baadhi ya mabenki, si kuzisakama benki hizo bali kuwaondoa katika usingizi mzito wa ulinzi kwani ujambazi kwa sasa jijini Dar hasa kwa wateja wanaotokea benki ni jambo la kutisha.

Tayari gazeti hili lina mlolongo wa wateja waliopigwa risasi na kufa wakiwa wanatoka ndani ya benki kuchukua fedha. Swali ni je, majambazi hao huwa wanaambiwa na nani kwamba, mteja anayetoka amebeba ‘mzigo mnono’?

Gazeti hili linamshauri Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova kusimamia suala hili kwa karibu ili kupunguza matukio ya ujambazi katika benki
CHANZO:GLOBAL
Older Posts
© Copyright VIJIMAMBOZI Published.. Blogger Templates
Back To Top