Lulu Atoboa Sababu ya Kutofanya ‘Movie’kwa Mwaka Mzima


Staa wa Bongo Movies, Elizabeth Michael,’Lulu’amefunguka sababu ya kutofanya filamu kwa mwaka mzima kuwa alikuwa bize na shughuli zingine ikiwemo masomo.

Akizungumza na Clouds Fm,alisema kuwa mwaka jana wote alikuwa ‘host’ kwenye mashindano ya kutafuta vipaji vya uigizaji (Tanzania Movie Talents) ambayo ilifanyika karibu mikoa yote,pia alikuwa bize na masomo katika chuo cha Magogoni akichukua kozi ya Public Administration.

‘’Mwaka jana wote sikufanya filamu kabisa kutokana na kuwa bize kwenye shindano la kutafuta vipaji vya uigizaji na pia shule nayo ilinibana kwahiyo sikuwa na muda wa kufanya filamu,’alisema Lulu.

Aidha alisema kuwa kwa sasa ameingia mzigoni kufanya filamu yake mpya ambayo hajaipa jina bado chini ya kampuni yake ya Proin Promotion ambayo itakuwa na wasanii mbalimbali kama Dude na wengineo.

‘Filamu hii inahusu maisha,mapenzi na komedi kidogo na kwa sasa hivi nitakuwa natoa filamu mbili kwa mwaka ndiyo utaratibu niliojiwekea,’aliongeza Lulu.

Cloudsfm.com

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright VIJIMAMBOZI Published.. Blogger Templates
Back To Top