Staa mkongwe kwenye uchekeshaji, Kingwendu amesema kuonekana kwenye video za muziki za wasanii ni moja ya biashara zake anazozipa uzito.
Kingwendu ameonekana kwenye video kadhaa ikiwemo ile ya wimbo wa Yamoto Band.
Akiongea na 255 ya XXL kupitia kituo cha redio cha Clouds FM, Kingwendu alisema kabla hajakubali kufanya video, huangalia kwanza wimbo huo una ujumbe gani.
“Inategemea kwanza na video gani, kama ni movie au muziki kama muziki, naangalia kwanza ameimba nini na huo wimbo una ujumbe gani. Mfano ujumbe kama wa wimbo ule wa Yamoto Band,” alisema.
“Video ya muziki nafanya kuanzia laki tano hadi milioni moja hiyo ni kwa underground, hapo atakuwa amelialia ndio nawafanyia bei hiyo. Ila supastar mwenzangu namfanyia bei rahisi maana najua ipo siku na miye nitamwitaji. Cha muhimu tufanye tu kazi kwa ushirikiano.”
Bongo5
Post a Comment