Jumatatu ya April 06 kati ya stori zilizosikika kwenye uchambuzi wa MAGAZETI kwenye #PowerBreakfast iko ya Askofu Gwajima kusema hawezi kuwatupa Lowassa na Dk. Slaa kwa
kuwa ni marafiki zake wa siku nyingi, UKAWA kuidai Serikali mambo manne
kabla ya uchaguzi, na madereva kugoma kurudi shule kwa kuwa hawana
mikataba ya ajira wanazofanya.
Stori nyingine inahusu mtoto mlemavu
kufungiwa darini miezi minne, Polisi kujiua kwa kujipiga risasi katika
kituo cha Polisi Tabora, iko nyingine ya waasisi wa CCM kukubali utafiti
ulioonesha Prof. Mark Mwandosya anafaa kugombea Urais 2015.
Rais Kikwete amesema Serikali ya awamu yake inajivunia mafanikio, Waziri Bernard Membe amewataka vijana wasikubali kutumika, kuna stori pia ya watu 1665 kukosa makazi kutokana na mvua kubwa iliyonyesha Simiyu.
Imeandikwa pia kuhusu bunduki nyingine
kupotea katika mazingira ya kutatanisha kituo cha Polisi Tabora, watoto
21 wazaliwa katika mkesha wa Pasaka Iringa, wapenzi waliokamatwa kwa
kuuza tiketi za kwenda peponi Uingereza na waumini Shinyanga wakaguliwa
kabla ya kuingia kwenye ibada ya mkesha wa Pasaka.
Hizi zilisikika kwenye show hiyo..
88.1 Clouds FM inasikika ukiwa Mwanza.
Kama ulipitwa bonyeza play hapa chini kusikiliza uchambuzi wa story zote za Magazeti ya leo…SIKILIZA HAPA
Post a Comment