Kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano kukojoa kitandani au kujikojolea ni jambo la kawaida, lakini vijana na watu wazima kujikojolea kitandani mara kwa mara siyo jambo la kawaida katika jamii.
Kitabu cha afya ya akili kilichotolewa na Chama cha Madaktari wa magonjwa ya akili cha Marekani kinasema kuwa kikojozi ni mtu mwenye tatizo la kujikojolea nguoni au kitandani angalau mara mbili kwa wiki kwa muda wa miezi mitatu mfufulizo akiwa na umri wa miaka mitano au zaidi.
Tafiti zinaonyesha kwamba katika kila watu wazima 100, mmoja wao ni kikojozi na kwa upande wa Tanzania, hivyo inayokadiriwa kuwa na Watanzania milioni 50 idadi ya watu wazima vikojozi inakadiriwa kuwa ni sawa na nusu milioni.
Wengine wanahusisha tatizo hili na matatizo ya mishipa ya fahamu kushindwa kumpatia muhusika taarifa ya kujaa kwa kibofu pindi anapokuwa usingizini na sababu nyingine ni uwezo mdogo wa kibofu kushindwa kubeba mkojo wa kutosha kutokana na kulegea kwa valvu zake.
Sababu za tatizo hili ni pamoja na kukomaa kwa tezi ya pituitary inayopatikana ndani ya ubongo ambapo ikikomaa husababisha figo kuzalisha kiasi kikubwa cha mkojo na matokeo yake muhusika akiwa usingizini hupoteza uwezo wa kuudhibiti.
Chanzo cha story: Gazeti la Mwananchi, Toleo la January 16, 2015.
Post a Comment