Mwanamke mmoja nchini Marekani amejifungua mtoto mwenye uzito wa paundi 14.1 sawa na kilo 6.4kg na sasa mtoto huyo anakula mara mbili zaidi ya uwezo wa mtoto mchanga.
Bi Maxxzandra Ford amepata mtoto aliyempa jina Avery, ndiye mtoto mkubwa na mzito kuwahi kuzaliwa katika hospitali ya wanawake ya mtakatifu Joseph iliyoko Tampa, Florida.Avery, alizaliwa kwa njia ya kawaida.
Ford alikuwa hajatanabahi kuwa yu mjamzito mpaka alipotimiza wiki 35 .lakini mara baada ya kuwa anaongezeka uzito kupita kiasi ,madaktari wakamthibitishia kuwa yu mja mzito,na kutokana na kasi ya unenepaji mwanzo Bi Ford alihisi atajifungua watoto pacha,kumbe sivyo.
Debbie Moore, mkunga katika hospitali hiyo, wasingemruhusu mwanamke huyo ajifungue kwa njia ya kawaida kama wangegundua mapema ana mtoto mwenye kilo nyingi kiasi hicho .
Avery anabaki hospitalini chini ya uangalizi maalumu tangu alipozaliwa tarehe 29 January , lakini anatarajiwa kuruhusiwa kwenda nyumbani hivi karibuni.Bi Ford, anaye mtoto mmoja mwenye umri wa mwaka mmoja na mtoto wa kike mwenye miaka mitano.
(Chanzo: BBC)
Post a Comment