LAANA:SALUNI YA NGONO YAFUMULIWA HUKO DAR

 
HALI ni mbaya! Wakati suala la ajira likiwa bado ni kitendawili kikubwa kwa serikali, Jiji la Dar hivi sasa linatisha, baada ya watu kubuni mtindo mpya wa kujipatia fedha kwa kujihusisha na biashara haramu ya ngono katika maeneo yanayotambulika kufanya shughuli nyingine halali, Risasi Jumamosi lina mkanda mzima.

Mhudumu wa saluni ya kuchua akitweta mara baada ya kunaswa na OFM akijihusisha na biashara haramu ya ngono.

UCHUNGUZI
Makachero wa kitengo maalum cha Global Publishers cha Operesheni Fichua Maovu (OFM) walifanya uchunguzi na kugundua kuwa zipo saluni nyingi jijini Dar zinazojishughulisha na biashara ya massage (kuchua) lakini ndani yake wahudumu wanajiuza hadi miili ambapo wateja wakubwa ni waume za watu na vigogo serikalini.

Kikosi kazi cha OFM kikimtaiti mhudumu huyo.

TUKIO BICHI
Hivi karibuni OFM walipokea simu kutoka kwa mmoja wa wanawake aliyedai kuchoshwa na shughuli zinazofanyika katika saluni moja ya kuchua (massage, jina linahifadhiwa kwa sasa) iliyopo katika eneo la Kinondoni-Morocco, Dar.

Mhudumu huyo mwenye asili ya kisomali akitinga viwalo mara baada ya kunaswa katika mtego wa OFM.

“Jamani nipo hapa nje, nimemfuatilia mume wangu, maana kila siku nasikia huwa anaonekana hapa, hii ni saluni ya kuchua, lakini humo ndani wale wahudumu ni makahaba, wanajiuza tena wanafanyia humohumo ndani, naombeni mje, nataka kufumania,” chanzo chetu kiliongea kwa hasira na uchungu.

...Huyu hapa ndio mhudumu mwenyewe.

OFM MZIGONI 
Kama ilivyo kawaida ya OFM kutodharau wito wowote unaohusiana na uvunjaji wa maadili, uonevu na uhalifu, kikosi kilipangwa harakaharaka na kwa kutumia pikipiki ziendazo kasi, zikafika eneo la tukio katika muda muafaka, kwani difenda la polisi, nayo ilionekana ikiingia eneo hilo kuitikia wito wa raia wema.

Baadhi ya vifaa vya kufanyia masaji vikiwa mezani.

KABAAAH!
Ndani ya saluni hiyo, OFM ilishuhudia mhudumu wa mapokezi ambaye baada ya kuonyeshwa vitambulisho vya askari wa Jeshi la Polisi, alinywea na kuwaruhusu kupekua chumba kimoja baada ya kingine, ili kujionea kama kweli nyumba hiyo ilikuwa ikijihusisha na masuala ya saluni ya uchuaji pekee na siyo vinginevyo.

Moja ya vitanda vinavyotumiwa kwa ajili ya biashara ya ngono kwa wateja wanaofika katika saluni hiyo.

Katika chumba cha kwanza, askari hao walimkuta mwanaume mmoja akiwa uchi wa nyama, lakini mwanamke aliyekuwa naye akiwa amevaa nguo zake, kitu kilichoashiria kuwa tayari ‘mchezo ulishafanyika’.
Katika hali isiyotarajiwa, baada ya kupitia vyumba vingine vinne na kuvikuta tupu, kilichofuata, OFM walishuhudia mwanamke mwenye asili ya Kisomali akiwa uchi na mwanaume wake, dalili zote zikionyesha kuwa walikuwa wakijiandaa kufanya uzinzi.

Mhudumu mwingine aliyenaswa katika saluni hiyo.

WAZINZI WAJITETEA
Baada ya kuwakuta katika hali hiyo, kiongozi wa askari hao, (jina kapuni) aliwauliza kama hiyo ndiyo biashara ya masaji waliyopata kibali cha kuifanya, lakini wakabakia kujiumauma pasipo kutoa jibu la kueleweka.
Binti huyo wa Kisomali, ghafla aliibuka na kuanza kuomba msamaha kwa kitendo hicho, akidai maisha magumu wanayoishi, ndiyo yanayosababisha waifanye biashara hiyo.

Wahudumu walionaswa wakipakizwa kwenye karandinga kuchuliwa hatua za kisheria.

KUMBE ANA MTOTO
Lakini la kushangaza zaidi, ni pale mwanamke huyo alipodai kuwa nyumbani alikotoka, ambako ameolewa, pia alimuacha mwanaye mwenye umri wa miezi minne.

“Nisameheni jamani, mimi ni mke wa mtu na isitoshe nimeacha kichanga nyumbani, ni shida tu ndiyo imenileta hapa,” alisikika akiomba mwanamke huyo aliyejitambulisha kwa jina moja la Salma.
Mwanaume aliyekutwa naye, alipoulizwa biashara hiyo inafanyika kwa bei gani, alisema makubaliano yake na mwanamke huyo, ni kutoa kiasi cha shilingi elfu sitini kwa tendo moja!
OFM iliondoka eneo hilo baada ya askari hao kuwapakiza katika karandinga wanawake wanne na wanaume wawili tayari kwa safari ya kituoni kwa ajili ya hatua zaidi za kisheria.
CHANZO:GLOBAL PUBLISHER

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright VIJIMAMBOZI Published.. Blogger Templates
Back To Top